6/13/18

FAHAMU MBEGU ZA NYONYO/MBARIKA

Utangulizi

Mbarika ama nyonyo (castor seeds) ni mbegu za daikotiledoni ambazo zipo katika kundi la mbegu zitoazo mafuta, kundi moja na mbono kaburi (jatropha). Mmea wa nyonyo kitaalamu hujulikana kama 'ricinus communis'. Katika jamii nyingi za Kiafrika, mbegu za mmea huu zimekuwa zikitumika kutengeneza mafuta kwa ajili ya kulainisha ngozi za wanyama na kuwashia taa.
Mimea ya nyonyo ni sumu, kwa hivyo hailiwi na wanyama na husitawi maeneo mengi, hata yale yaliyo na ukame.

Picha: Mmea wa nyonyo/mbarika

Picha: Mbegu za nyonyo/mbarika, kabla hazijakomaa.

MATUMIZI

Mmea wenyewe hutumika kama uzio hai (live fence)
Katika baadhi ya jamii, majani ya mmea huu hutumika kukanda (massage) na kutibu maumivu yatokanayo na kuteguka.
Mbegu za nyonyo husagwa, huchemshwa na kuenguliwa mafuta. Mafuta ya nyonyo huweza kusafishwa katikaa mitambo ya kisasa na kutumika kuendeshea mitambo kama dizeli ya mimea (biodiesel). Pia hutumika kutengenezea mafuta ya kulanisha mitambo. Kumbuka kuwa mafuta ya kulainisha mitambo aina ya Castrol hutengenezwa kutokana na mmea huu.

3 comments:

John Mwaipopo said...

Mzee nilikuwa sijatembelea blogu siku nyingi imekolea kinoma. Itafunika sana hii.

mwalyoyo said...

Sawa mkuu PF, tuendelee kuiboresha!

john joseph tesha said...

Elimu nzuri, je hulimwa wapi na upatikanaji wa Mbegu upoje