8/17/06

NIKO UPANDE WA PILI WA KIJIJI CHETUMu hali gani wana blogu wenzangu?
Mimi mzima kabisa na kwa sasa nablogu tokea upande wa pili wa dunia, ambayo tunasema kuwa sasa ni kama kijiji. Sasa basi, mimi nipo upande wa kaskazini wa kijiji chetu (dunia). Nipo jijini Oslo nchini Norway. Nitaendelea kublogu tu hata huku, pamoja na kwamba majukumu ni mengi kazini. Nitawagawia kile nitakachojifunza huku bila choyo.

1 comment:

mwaifwanic said...

Kutoka huko upande wa pili wa dunia tuambie wenzetu wanakabiliana vipi na changamoto za mazingira duniani. Kwa vile nchi yao ni ndogo je wanaweza vipi kudhibiti mlipuko wa ongezeko la watu (population explosion) ambalo ni chanzo kimojawapo cha uharibifu wa mazingira. Vile vile Norway ndiko nyumbani kwa vilongalonga vyenye nembo ya NOKIA, tuambie wamewezaje kuyapiku mataifa makubwa kiuchumi katika kuhakikisha kuwa wao ndiyo wenye tenolojia bora kuliko zote ya mawasiliano ya kiganjani?