U hali gani mpenzi msomaji wa blogu hii?
Ningependa kuongelea suala muhimu sana katika maisha yetu ya uanazuoni. Mwaka jana Desemba 30, 2005 wakati rais wetu anahutubia bunge la Jamhuri ya Muungano (wa Tanzania?) kwa mara ya kwanza, aligusia kwa uchungu sana suala la wanataaluma kutotumia ipasavyo taaluma yao, lakini yeye aliita "Kutukanisha Taaluma" Katika mfano mmojawapo, aliwatuhumu Mabwana (nafikiri na Mabibi) ardhi kuwa wanauza maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya michezo, ili yatumike kwa shughuli za ujenzi, wakati taaluma yao hairuhusu kufanya hivyo.
Ukiliangalia suala hili kwa undani, utaona ukweli wake, hasa ukifuatilia suala la migogoro ya ardhi katika Tanzania, wilaya ya Kinondoni ikiongoza. Inasemekana kuwa hakuna wilaya yenye migogoro mingi ya ardhi katika Jiji la Dar es salaam kama Kinondoni. Zingatia kuwa karibu asilimia kubwa ya nyumba za bei mbaya kwa jiji hili ziko kinondoni ukianzia na Mbezi beach, Masaki, Oysterbay, Kinondoni nk. Hili la watu wa ardhi ni kundi moja la 'watukanisha taaluma'.
Kundi jingine alilogusia Mheshimiwa Rais ni la wanasheria, ambao hujigamba kwa kujiita "Learned Brothers/Sisters". Hawa nao hawajambo kwa kusaini mikataba ya ajabu ajabu ambayo ni wengi wetu tunaifahamu na inatukera. Ni hawa hawa waliosaidia kupitisha kwa kishindo sheria ya takrima, ambayo, kwa sasa wanataaluma wasiokubali kutukanisha taaluma yao wamesema kuwa haifai. Hebu tujiulize, iweje msomi wa shahada kadhaa za sheria akatia sahihi ya kuipitisha sheria ambayo anajua (au hajui?) kuwa inakiuka katiba ya nchi? Utajiitaje msomi ikiwa huthamini elimu na maadili ya taaluma yako?
Kuna kundi jingine la wanataaluma wanaotukanisha taaluma yao. Hawa ni wale ambao waliruhusu ujenzi wa majengo marefu sana pale Jijini Dar, hasa Kariakoo bila majengo hayo kukidhi viwango vya kitaalamu vinavyotakiwa. Matokeo ya kutukanisha taaluma yao tunayaona sasa, ambapo majengo kadhaa yameamriwa kubomolewa, kwa kuwa hayakidhi viwango sahihi vya ujenzi. Ina maana kuwa kabla ya majengo haya kujengwa hayakukaguliwa kama yanakidhi viwango vinavyotakiwa? Hivi hawa nao wanaithamini taaluma yao?
Hivi, ni viwanda vingapi hapa Tanzania ambavyo vinazingatia usalama wa mazingira kwa kushughulikia taka zizalishwazo na viwanda hivi? Wataalamu wa Tathmini za Athari za Mazingira (EIA) mpo? Mnatumia taaluma yenu kama ipaswavyo? Mmeona rangi ya maji ya mto Kizinga pale Mbagala Mission? Na rangi ya mto Kiwira pale Ilima Rungwe ikoje? Mmechukua hatua gani?
Kuna mambo mengi sana ya kuongela kuhusu uhusika wetu katika taaluma zetu, lakini hasa tujiulize, ni kwa nini baadhi yetu 'tunatukanisha' taaluma zetu? Mpaka hapo, ni kwa nini vyeti vya elimu ya hawa watukanishaji taaluma isitiliwe mashaka? Je hayo ni matokeo ya "kudesa?" au kuzunguka mbuyu?
Ni kwa kiasi gani tunathamini taaluma zetu?
Jadili
Blogu hii ipo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu masuala mbali mbali ndani ya jamii hii pana, hasa masuala ya mazingira, nishati na maendeleo endelevu. Ingawa taarifa zilizo katika tovuti hii zinatolewa bure kwa ajili ya kuongeza uelewa katika jamii,si vibaya kama utataka kunakili ama kuzitumia, ila ni vyema na ni ustaarabu kama utataja kuwa umezitoa hapa. Asante
5/26/06
5/22/06
UKO HURU KUNENA!
Karibu katika blogu hii. Hapa tutakuwa tukijadili mada mbali mbali pamoja na kutoa maoni katika mada husika.
Zingatia kuwa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (toleo la 1998) sura ya kwanza sehemu ta tatu, ukurasa wa 23 ibara ya (18) (1) kinachohusu uhuru wa mtu kutoa mawazo yake , kinatamka bayana kuwa 'bila kwenda kinyume cha sheria za nchi, kila mtu ana haki na uhuru wa kutoa mawazo/fikra zake, na kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa au fikra kwa kutumia njia yeyote ile, bila kujali mipaka ya nchi na ana haki ya ya kutoingiliwa katika mawasiliano au mpashano huu wa habari'. (2) 'Kila raia ana haki ya kupashwa habari muda wote kuhusu matukio mbali mbali katika nchi na dunia kwa ujumla wake, ambayo ni muhimu kwa watu na maisha yao na muhimu kwa jamii nzima pia.'
Hivyo basi, ni kwa kutumia uhuru huu ambapo blogu hii inafanya kazi , na ndugu msomaji/mchangiaji upo huru kuchangia mawazo yako kwa mada tutakazokuwa tunaziweka hapa.

Subscribe to:
Posts (Atom)