Blogu hii ipo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu masuala mbali mbali ndani ya jamii hii pana, hasa masuala ya mazingira, nishati na maendeleo endelevu. Ingawa taarifa zilizo katika tovuti hii zinatolewa bure kwa ajili ya kuongeza uelewa katika jamii,si vibaya kama utataka kunakili ama kuzitumia, ila ni vyema na ni ustaarabu kama utataja kuwa umezitoa hapa. Asante
10/3/12
Tanesco na ombi la maboresho kutoka kwa walaji (Consumers)
Utangulizi
Ofisi ya mahusiano ya Tanesco imetoa tangazo (pichani) ikiomba maoni ya wateja kuhusu maboresho ambayo wanataka kuyafanya, ili kuongeza ufanisi wa shirika hilo. Shirika hili ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi, hivyo ufanisi wake ni nguzo muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi wetu kwa ujumla.
Ushauri
Mimi ni mdau wa nishati katika taifa hili na pia ni mteja wa Tanesco. Kuna mada fulani (iko hapa) niliiweka katika blog hii siku za nyuma kuhusu matatizo yanayoisibu Tanesco na namna ya kupunguza kama si kuondoa kabisa matatizo hayo. Tanesco ina vitengo vitatu muhimu, ambavyo ni uzalishaji umeme (Generation), usafirishaji umeme (Transmission) na ugavi umeme (Distribution). Shida kubwa sana ya Tanesco ipo katika generation na distribution. Ningeomba watendaji wakuu (menejimenti na bodi)za shirika hili wazingatie ushauri niliowapa hata robo tu,watafikia hilo lengo wanalolitafuta. Ushauri wangu umewahi kutolewa na wataalamu wengine wengi tu akiwamo Januari Makamba. Lakini pia wasome (na ikiwezekana kutekeleza) mapendekezo ya ripoti iliyoandaliwa na Benki ya Dunia kuhusu upotevu wa umeme.
Ni hayo tu. Tuendelee na mjadala
Subscribe to:
Posts (Atom)